Skip to main content
U.S. flag

An official website of the United States government

Mzunguko Wa Maji - The Water Cycle, Kiswahili

Mzunguko wa maji unaelezea mahali maji yanapopatikana duniani na jinsi yanavyosafiri. Matumizi ya maji ya binadamu, matumizi ya ardhi, na mabadiliko ya hali ya hewa yote huathiri mzunguko wa maji. Kuelewa athari hizi kunaweza kusaidia kufanikisha matumizi endelevu ya maji.

•  Water Science School HOME  •  Water Cycle Diagrams

Media
Earth, the water planet
Ikitazamwa kutoka angani, kipengele kinachovutia zaidi cha sayari yetu ni maji. Katika hali ya kioevu na iliyoganda, inashughulikia 75% ya uso wa Dunia. Inajaza anga na mawingu. Maji yapo karibu kila mahali duniani, kuanzia ndani ya ukoko wa miamba ya sayari hadi ndani ya seli za mwili wa binadamu (NASA). Kilicho muhimu kukumbuka ni kwamba maji haya yote yanasonga kila mara katika sayari yetu.

Credit: NASA

Mzunguko wa maji ni nini?

Mzunguko wa maji unaelezea mahali maji yanapopatikana duniani na jinsi yanavyosafiri. Maji yanaweza kuhifadhiwa katika angahewa, juu ya uso wa dunia, au chini ya ardhi. Yanaweza kuwa katika hali ya kimiminika, kigumu, au gesi. Maji husogea kiasili na pia kutokana na mwingiliano wa binadamu, mambo yote mawili yakiwa na athari kwa mahali maji yanahifadhiwa, jinsi yanavyosafiri, na usafi wake. 
 

Mabwawa huhifadhi maji

Maji ya kioevu yanaweza kuwa safi, chumvi, au mchanganyiko (maji ya chumvi hafifu). Asilimia tisini na sita ya maji yote ni yenye chumvi na yanahifadhiwa katika bahari. Maeneo kama bahari, ambapo maji yanahifadhiwa, huitwa hifadhi za maji. Juu ya ardhi, maji yenye chumvi huhifadhiwa katika maziwa ya chumvi, ilhali maji safi  huhifadhiwa ikiwa katika hali ya kioevu kwenye maziwa ya maji safi, mabwawa za bandia, mito, ardhi oevu, na kwenye udongo kama unyevu wa udongo. Chini zaidi ya ardhi, maji ya kumiminika huhifadhiwa kama maji ya chini ya ardhi kwenye chemichemi za maji, kwenye nyufa na kwenye mashimo ya miamba. Aina ngumu na iliyoganda ya maji huhifadhiwa katika tabaka za barafu, barafu ya mwandamo (glasia), na tabaka za theluji iliyokusanyika katika maeneo ya juu au karibu na ncha za dunia.  Maji yaliyogandishwa pia hupatikana kwenye ardhi kama udongo wenye barafu ya kudumu. Mvuke wa maji, maji katika hali ya gesi, huhifadhiwa kama unyevu wa anga juu ya bahari na juu ya nchi kavu.
 

Media
A rainstorm providing water to crops with a sunset in the background
Mawingu huundwa kwa kuganda kwa maji katika angahewa. Maji yanaporudishwa kwenye uso wa Dunia tunapata mvua. Ufupishaji na kunyesha ni mabadiliko muhimu katika mzunguko wetu wa maji.

Credit: Tobias Hämmer | Pixabay

Mtiririko wa maji huhamisha maji kati ya Hifadhi za maji

Maji yanaposafiri, yanaweza kubadilika na kuwa kimiminika, kigumu, au gesi. Njia tofauti ambazo maji husafiri kati ya hifadhi zinajulikana kama mtiririko wa maji. Mzunguko huchanganya maji katika bahari na husafirisha mvuke wa maji katika angahewa. Maji husafiri kati ya anga na uso wa dunia kupitia uvukizaji, mvuke mnyunyizo, na mvua.  Juu ya uso wa ardhi, maji husonga kupitia myeyuko wa theluji, mtiririko wa maji juu ya ardhi, na mtiririko wa maji kwenye mito. Maji hungia ndani ya ardhi kupitia usafirishaji wa maji ardhini na uongezaji wa maji ya chini ya ardhi.  Yakiwa chini ya ardhi, maji husafiri kwenye tabaka za maji na yanaweza kurudi juu ya uso wa ardhi kupitia chemchemi au kwa utokaji wa asili wa maji na kuingia kwenye mito na bahari.
 

Wanadamu hubadilisha mzunguko wa maji

Media
Reservoir behind dam structure depicting human influence on the water cycle
Hifadhi ni ziwa lililoundwa na mwanadamu. Mabwawa hutengenezwa wakati bwawa limejengwa juu ya mto, na kuruhusu maji kukusanyika nyuma ya bwawa.

Credit: Thomas Ehrhardt | Pixabay

Tunaelekeza mito upya, tunajenga mabwawa ili kuhifadhi maji, na tunakausha ardhi oevu kwa ajili ya maendeleo. Tunatumia maji kutoka kwenye mito, maziwa, mabwawa ya hifadhi, na tabaka za maji ya chini ya ardhi. Tunatumia maji hayo kwa madhumuni yafuatayo: 1) Kusambaza maji kwa matumizi ya nyumbani na jamii. 2) Kwa umwagiliaji wa kilimo na malisho ya mifugo. 3) Katika shughuli za viwanda kama uzalishaji wa nishati ya umeme wa joto, uchimbaji madini, na ufugaji wa samaki. Kiasi cha maji kinachopatikana hutegemea kiasi kilicho katika kila hifadhi (kiwango cha maji). Upatikanaji wa maji pia hutegemea muda na kasi ya usafirishaji wa maji (muda maji yanasonga), kiasi cha maji kinachotumika (matumizi ya maji), na ubora wa maji (usafi wa maji).

Shughuli za binadamu huathiri ubora wa maji. Katika maeneo ya kilimo na mijini, umwagiliaji wa maji na mvua husomba mbolea na viuatilifu hadi kwenye mito na kwenye maji ya chini ya ardhi. Mitambo ya umeme na viwanda hurudisha maji yenye joto na machafu kwenye mito. Mtiririko wa maji juu ya ardhi hubeba kemikali, mashapo, na maji taka hadi kwenye mito na maziwa. Chini ya aina hizi za vyanzo, maji yaliyochafuliwa yanaweza kusababisha makuzi hatari ya mwani, kusambaza magonjwa, na kuharibu makazi ya viumbe.
 

Mzunguko wa maji na mabadiliko ya hali ya hewa

Mabadiliko ya hali ya hewa pia yanaathiri mzunguko wa maji. Yanaathiri ubora wa maji, kiwango  au wingi wa maji, muda wa usafirishaji, na matumizi ya maji. Zaidi ya hayo, mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha ongezeko la asidi baharini, kupanda kwa kina cha bahari, na hali mbaya ya hewa. Kuelewa athari hizi kunaweza kusaidia kufanikisha matumizi endelevu ya maji.
 

Mchoro wa mzunguko wa maji

Mzunguko Wa Maji (PNG | PDF)                                                        Mchoro Wa Mzunguko Wa Asili Wa Maji (JPG | PDF)

Media
A landscape depicting where water is (in bright blue) and how it moves (with arrows). Human activities are shown throughout.
Media
Mzunguko wa maji - The Natural Water Cycle, Swahili
Was this page helpful?